Top Stories

Rais Samia kufanya ziara ya siku mbili nchini Kenya

on

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini Kenya siku ya Jumanne.

Rais Samia atakuwa katika ziara nchini humo kwa siku mbili ambapo atapokelewa na mwenyeji wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, imeeleza Ikulu ya Kenya.

Hii ni safari ya pili kwa rais Samia tangu alipoapishwa kuchukua madaraka baada ya kifo cha Hayati Dk. John Magufuli.

Awali, alifanya safari yake ya kwanza kama Rais nchini Uganda Aprili 11, Mwaka huu na Rais Yoweri Museveni akielezea kuwa lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili na kumaliza makubaliano ya mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka nchini Uganda kuja Tanga, Tanzania.

MEI MOSI: “TULIKUJA NA MATARAJIO YAKUONGEZWA, HATA KWA PUNGUZO TUNASHUKURU”

Soma na hizi

Tupia Comments