Habari za Mastaa

NOMAA!! Nandy aendelea kung’ara 2019, hili ndilo gari jipya aliloongeza

on

Star wakike wa Bongofleva Faustina Charles maarufu kamaNandy ameendelea ku – shine 2019 ambapo time hii amezidi kuonesha mafanikio yake kupitia muziki kwa kuonesha gari lake jipya alilonunua hivi karibuni, Nandy ameionesha gari hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwenye Insta – story kwa kupost video akilionesha hilo gari na namba zake mpya.

Gari hilo alilonunua Nandy ni aina ya Toyota Alphard inayokadiriwa kuwa na thamani ya million 16 mpaka 17 huku ikiwa tayari anamiliki magari mengine mawili aliyowahi kuyaweka hadharani ambayo ni Mercedes Benz E-Class E320 CDI na BMW X1 na hapo awali msanii huyo aliwahi kutumia gari aina ya Toyota Harrier.

 

EXCLUSIVE: RUBY KAFUNGUKA, KATAJA JINSIA YA MTOTO WAKE “NDOA VERY SOON”

Soma na hizi

Tupia Comments