Habari za Mastaa

Msanii aliyepata upofu baada ya kuwekewa Drip11 Hospitali “Nina miaka 7 sioni””

on

Steven Mkami ni msanii wa muziki wa Gospel ambaye amepoteza uwezo wa kuona kwa miaka saba mpaka sasa ambapo amedai tatizo hilo lilisababishwa na matatibabu aliyokuwa akipewa wakati alipougua ugonjwa malaria.

Steven amesema chanzo ni kuwekewa drip nyingi ambazo amezikadiria kufika kumi na moja, pia ameongeza kuwa amezaa watoto wa nne na mke wake ila mtoto aliyebahatika kumuona ni mmoja tu ambaye alimuona akiwa na miezi sita tu.

Pamoja na hayo Steven ameelezea jinsi anavyofanya shughuli zake za muziki wa kumtukuza Mungu ingali akiwa haoni na kueleza inavyokuwa wakati akishoot video za nyimbo zake na hata njia anayotumia kurecord wimbo studio bila kuandika mahali.

Bonyeza PLAY hapa chini kutazama FULL VIDEO.

 

VIDEO: PRODUCER LAMAR NA MONA GANSTER WAZUNGUMZA “LAZIMA TULIPWE”

Soma na hizi

Tupia Comments