Kijana Aaron Patrick Aadkin (16) ni kijana mwenye ndoto za kutoboa kisoka, ndoto hiyo haikuishia tu kitandani bali jitihada zake zimeanza kuonekana na Wazazi wake kama baba yake Patrick Aadkin ameanza kumsapoti na kumtilia mkazo.
Aaron amerejea Tanzania hiyo ni baada ya kumaliza majaribio yake katika Klabu ya Juventus ya Italia ambapo alikwenda kwa wiki moja.
Juventus wana academy nchini na huwachukua baadhi ya vijana kwenda nje kuwafuatilia na Aaron alikuwa mmoja wao na sasa amerejea anashea na sisi aliyokutana nayo.