Mix

Aaron Ramsey nje ya dimba kwa wiki 6

on

Barclays-Monthly-Awards-Ramsey-Wenger-2349564

Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey hatoweza kuitumikia klabu ya Arsenal kwa takribani wiki sita, meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger amesema.

Ramsey ambaye amekuwa fomu nzuri msimu, tayari alishakuwa nje ya dimba kwa takribani mwezi mmoja sasa baada ya kuumia katika mchezo wa ushindi wa 3-1 dhidi ya West Ham mnamo mwezi December.

Akiongea na waandishi wa habari muda mchache uliopita Wenger alisema: “Aaron Ramsey atakuwa nje ya dimba kwa wiki nne mpaka sita sasa.”

Wakati huo huo Wenger amekanusha mpango wa  klabu hiyo kutaka kumsajili kiungo wa Schalke Julian Draxler.

Tupia Comments