Manchester City imefikia makubaliano na klabu ya Lens kwa usajili wa beki Abdukodir Khusanov kwa ada ya pauni milioni 33.5 zaidi ya tsh. bilioni 100.
Hatua hii inaonyesha dhamira ya City kuimarisha kikosi chao katika dirisha hili la usajili.
Khusanov anayejulikana kwa uwezo wake wa kucheza nafasi mbalimbali kwenye safu ya ulinzi na anatarajiwa kuleta nguvu mpya kwenye kikosi cha Pep Guardiola.
Usajili huu ni sehemu ya mipango kabambe ya klabu hiyo kuelekea msimu unaofuata.
Ripoti zinadai pia kuna malipo ya ziada ya bonasi yaliyoambatanishwa na mauzo hayo, huku mchezaji huyo akitakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wiki hii kabla ya uhamisho huo kuthibitishwa rasmi.