Michezo

Abromavich katangaza kuiuza Chelsea na pesa zote kutoa msaada

on

Bilionea wa Kirusi na mmiliki wa club ya Chelsea ya England Roman Abromavich amethibitisha kuwa anataka kuiuza club hiyo kwa maslahi mapana ya club, wadhamini na wafanyakazi wa club.

“Ningependa kutoa taarifa kuhusiana na tetesi zinazoendelea kwenye vyombo vya habari kuhusiana na umiliki wangu Chelsea, siku zote nimekuwa nikifanya maamuzi kwa sababu ya maslahi ya club, kwa hali inavyoendelea sasa nimeamua kuiuza club (Chelsea)”>>> Roman Abromavich

Roman aliinunua club hiyo 2003 kwa pound milioni 140 (Tsh Bilioni 433) na sasa ameamua kuiza kutokana na vikwazo vilivyowekewa Taifa lake la Urusi, kwa mujibu wa Forbes kwa sasa Chelsea ina thamani ya pound Bilioni 2.4 (Tsh Trilioni 7.4).

Roman katika taarifa iliyotolewa na Chelsea anasema atauza club hiyo na pesa zote alizouza zitaenda katika mfuko maalum wa kusaidia waathirika wa vita nchini Ukraine na wala hana lengo la kujipatia faida.

Soma na hizi

Tupia Comments