Imekuwa ishu kubwa kwenye vyombo vya Habari sasa hivi.. mfululizo wa ajali za barabarani kila mtu anapata maswali mengi, nini chanzo cha ajali hizo? Njia ipi itumike ili kumaliza tatizo la ajali??
Wakati hayo yakiendelea naipokea ripoti nyingine toka Shinyanga, inahusu ajali ya basi la Unique ambalo limegongana na lori, kwenye ajali hiyo watu 10 wamefariki.. zimepita siku chache tu toka itokee ajali ya Toyota Hiace ambayo iliua watu 19 Mbeya pamoja na kuporomoka kwa mgodi ambao ulifukia watu 19 Kahama.
#RIP kwa watu wetu.
Kwa taarifa zaidi kaa karibu na millardayo.com, pamoja na countdown ya AMPLIFAYA @CloudsFM ili nikufahamishe zaidi kuhusu ajali hii.
Stori iliyonifikia inahusu watu 10 kufariki wengine zaidi ya 40 kujeruhiwa ktk ajali ya basi la Unit lililogongana na lori Shinyanga. #RIP
— millardayo.com (@millardayo) April 22, 2015