Ajali

Ndege imeanguka Egypt na watu zaidi ya 200… chanzo? vifo? hiki ndio kilichonifikia (+Video)

on

Ni mara chache sana tunakutana na ripoti kuhusu ajali za ndege ukilinganisha na ajali za usafiri mwingine kama magari na meli… hiyo sifa imefanya usafiri wa ndege kupewa namba moja ya usafiri salama zaidi Duniani kwa muda mrefu !!

Ndege ya abiria iliyokuwa inamilikiwa na Russia imeripotiwa kupata ajali saa chache zilizopita, kulikuwa na ripoti tofauti kuhusu usalama wa abiria 224 ambao walikuwa ndani ya Ndege hiyo lakini Ubalozi wa Russia uliopo Egypt wamethibitisha vifo vya watu wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Plane Crush

Kati ya watu hao waliokuwemo, 217 ni abiria ambao ni raia wa Russia waliokwenda Egypt kwa mapumziko, pamoja na wafanyakazi saba ambao walikuwa wakihudumia ndani ya ndege.

Ndege hiyo ilitoka Egypt ikielekea St. Petersburg, Russia… ndege ilipotea na kutoonekana kwenye rada na muda mfupi baadae ikaanguka eneo la Sinai.

Moja ya taarifa ya kwanza iliyoripotiwa kama Breaking News na Kituo cha CNN ni hii hapa.

https://www.youtube.com/watch?v=4Hk1beCD0Ks

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments