Baada ya ajali iliyoua watu 32 Arusha wakiwemo watoto 29 wa shule ya msingi Lucky Vicent leo May 6, 2017, watu mbalimbali maarufu wameoneshwa kuguswa na taarifa hizo na kuandika hisia zao kupitia mitandao ya kijamii.
Nimesikitishwa na vifo zaidi ya 31 vilivyosababishwa na ajali mbaya iliyotokea Karatu.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema.
— Tundu Antiphas Lissu (@TunduLissu) May 6, 2017
Hii habari ya Karatu inasikitisha sana,vitu vibaya ambavyo havipo ndani ya uwezo wetu kuvizuia..Mungu awasitiri na azipe nguvu familia zao
— ChoirMaster… (@MwanaFA) May 6, 2017
Allah Awastiri Na Kuwasamehe Makosa Yao Wanafunzi Walofariki Kwenye Ajali Ya Basi Huko Karatu… Pole Kwa Ndugu Jamaa Na Marafiki.
— Salama Zalhata Jabir (@EceJay) May 6, 2017
Mungu azilaze mahala pema peponi roho za wadogo zetu na wote waliofariki katika ajali ya Karatu. Bwana alitoa na Bwana ametwaa ???
— MASANJA (@mkandamizaji) May 6, 2017
Mwenyezi Mungu azipokee roho za marehemu wote na awape Nguvu Wazazi,Walezi na Familia zote zilizopatwa na Msiba huu uliotokea KARATU ?
— Elizabeth Michael (@OfficialLizyM) May 6, 2017
VIDEO: Ni Tundu Lissu na Joseph Mbilinyi tena bungeni… TAZAMA KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI