Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afŕika anatoa wito wa kukomeshwa kwa mikopo inayotolewa kwa ajili ya kubadilishana mafuta na madini muhimu barani humo, ambayo yameziacha baadhi ya nchi za Afŕika katika mgogoŕo wa kifedha.
Akinwumi Adesina aliliambia shirika la habari la AP mikopo hiyo “ni mbaya tu, kwanza kabisa, kwa sababu huwezi kupanga bei ya mali ipasavyo.”
“Kama una madini au mafuta chini ya ardhi, unapataje bei ya mkataba wa muda mrefu? Ni changamoto,” alisisitiza Adesina.
Mabadiliko ya nishati mbadala na magari ya umeme yamesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya madini muhimu, kuendesha aina hizi za mikopo.
Adesina, ambaye Abidjan, taasisi yenye makao yake makuu nchini Ivory Coast inasaidia kufadhili maendeleo katika nchi za Afrika, alisema mipango hii inakuja na msururu wa matatizo.