Michezo

PICHA 4 za mwonekano wa Uwanja mpya wa Klabu ya AC Milan ukikamilika..

on

milan2
Klabu nyingi zinazochezea Ligi Kuu Ulaya, au Klabu zenye majina makubwa Duniani ni ajabu kukuta Klabu haina Uwanja wake wa nyumbani wa michezo.. Man United wana wao wa Old Trafford, Chelsea wako pale darajani Stamford Bridge.

Klabu ya AC Milan kwa sasa wanautumia San Siro Stadium kama uwanja wao wa nyumbani.. lakini good news kuhusu wao leo ni kwamba Klabu hiyo ipo katika harakati za kujenga uwanja wake mpya ambao utajengwa kisasa zaidi eneo la Portello, Jiji la Milan, Italy.

milan

Mwonekano wa Uwanja kwa juu

Uwezo wa Uwanja huu ni kuchukua mashabiki 48,000 tu kwa wakati mmoja, upo katikati ya majengo makubwa ikiwemo hoteli kadhaa pamoja na maduka ya huduma mbalimbali ambayo yamezunguka uwanja huo.

milan3Unaambiwa teknolojia imehusika sana hapa.. jinsi ambavyo utajengwa utawekewa soundproof ambazo zitazuia kwa kiasi kikubwa kelele za ndani ya Uwanja zisitoke nje na kukera watu wengine.

Milan Pitch

Mwonekano wa Uwanja kwa nje

Ramani ya Uwanja iko kwenye hii video pia..

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments