Ikiwa Rais Magufuli ametimiza mwaka tangu achukue madaraka ya kuongoza nchi huku sifa za utendaji wake zikienea Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. leo October 8 2016 chama cha ACT Wazalendo kimefanya mkutano mkuu wa kidemokrasia ambapo umewakusanya wanachama na wageni mbalimbali kutoka nchi na vyama marafiki kwa ajili ya kubadilisha uzoefu katika nyanja mbalimbali.
Mmoja wa walioalikwa katika mkutano huo ni mwenyekiti wa chama cha Labour Kenya, Ababu Namwamba, mbele ya waaandishi wa habari Namwamba ameulizwa jinsi Wakenya wanavyochukulia utendaji wa Rais Magufuli, Namwamba amesema…
>>>’kuna sifa zimeenea kule Kenya kumekuwa na harakati za kupambana na ufisadi, harakati za kupunguza gharama za shughuli za umma, jina lake liko kule linavuma kule Kenya lakini swali kuu katika fikra za wakenya ni kuwa haya mambo tunayoyasikia katika vyombo vya habari ni porojo au propanganda au ni masuala yanayobadilisha maisha ya Watanzania, ingawa sifa za Magufuli zinaenea huku na kule tungependa kuona mabadiliko halisi hapa Tanzania mfano takwimu za ufisadi umepungua, takwimu za kuonesha hali ya maisha ya mtanzania yamebadilika‘
ULIKOSA USHAURI WA KIONGOZI WA CHAMA CHA UPINZANI KENYA KUHUSU MGOGORO WA ZANZIBAR? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI