Top Stories

Walichokizungumza ACT Wazalendo kuhusu lawama za Afande Sele

By

on

Leo October 4, 2016 Chama cha ACT Wazalendo kimechukua headlines baada ya msanii Afande Sele ambaye ni mwanachama wa chama hicho kupost maneno ya kudai kuwa amekua haelewi matendo ya chama hicho.

Taarifa iliyotolewa na afisa habari wa ACT Wazalendo Abdalah Hamis imesema chama hicho kimeona alichokiandika Afande Sele na wamechukulia kama maoni ya mwanachama wa kawaida na wanayeheshimu maoni hayo hata kama sio sahihi wanayapokea na hawawezi kumchukulia hatua zozote kwasababu wamechukua ni kama maono yake.

>>>Yeye ametoa maoni kama mwananchi wa kawaida hivyo hatuwezi kumjibu kama chama kwasababu amelezea hisia zake na kama kutakua kuna ukweli tutafanyia kazi na kama hakuna ukweli basi tutazipuuza taarifa hizo: Msemaji:- ACT Wazalendo

ULIPITWA NA ALICHOKIONGEA AFANDE SELE KUHUSU PROFESA JAY KUIMBA SINGELI? NIMEKUWEKEA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments