Top Stories

Adaiwa kumuua mpenzi wake aliemtembelea

on

Msichana mwenye umri wa miaka 19 amekamatwa na Polisi katika Kijiji cha Thiba, Kaunti ya Kirinyaga nchini Kenya kwa madai ya kumuua Mpenzi wake wa kiume chanzo kikiwa ni Mpenzi wake huyo kumtembelea nyumbani kwao bila ruhusa.

Baba wa Marehemu John Kmani amesema Mtoto wake alichomwa na kisu na Mpenzi wake baada ya kuzuka ugomvi uliosababishwa na Kijana huyo kwenda nyumbani kwa Mpenzi wake bila kumpa taarifa, bado haijawekwa wazi kuwa Msichana huyo alikuwa anaishi mwenyewe au na Wazazi wake.

Mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Kiamaciri akisubiri kufikishwa Mahakamani.

Soma na hizi

Tupia Comments