Michezo

Umesikia kuhusu mchezaji aliyemtuhumu mama yake kumroga?

on

Emmanuel Adebayor would be a loss for Spurs should he decide to play in the Africa Cup of NationsWakati mambo yakiwa hayamuendei sawa kwenye klabu yake ya Tottenham Hotspur, mshambuliaji wa Kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor ametoa kali ya wiki kwa habari ambayo imetengeneza vichwa vya habari vingi katika ulimwengu wa michezo duniani.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal amesema kwamba mama yake mzazi na ndugu zake wamekuwa wakitumia uchawi dhidi yake ili kuhakikisha haendelei kucheza soka.

Adebayor alitofautiana na mama yake na kumfukuza mama huyo katika moja ya nyumba zake huko Togo na dada zake wamekaririwa wakisema kwamba mchezaji huyo hapokei simu zao.

Mtandao wa allsports.com wa Ghana umechapisha habari yenye kauli ya mmoja wa dada wa mchezaji huyo ambaye alisema; “Kwa hivi sasa mama yetu anauza mifuko, makufuri na vitu vingine katika mpaka wa Ghana na Togo.

Mama yetu hajamuona Adebayor kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na kaka amekuwa hapokei simu anapopigiwa na mama, mama hampigii simu ili kumuomba fedha, anataka tu kuongea na mwanae kwa sababu anampenda sana..”

Adebayor-and-mum

Lakini Adebayor amekaririwa akisema; “Nawezaje kuongea na mama ambaye yeye pamoja na dada zangu wamekuwa wakinifanyia vitendo vya kishirikina ili wanimalize kwenye kazi zangu?..”

Tupia Comments