Michezo

Huyu ndio nyota wa Taifa Stars aliyetoka Uingereza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chad

on

Good news kwa soka la Tanzania hususani katika kipindi hiki cha kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya taifa ya Chad wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika 2017 itakayofanyika Gabon.

Tayari kuna taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya Mansfield Town ya Ligi daraja la pili Uingereza Abdillahie Yussuf anaripotiwa kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Chad utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam Jumatatu ya March 28.

Yussuf_2797311

Kama ulikuwa hujui Abdillahie Yussuf amelelewa na katika klabu ya Leicester City ya Uingereza ambayo kwa sasa inanyemelea ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza kwa kuongoza Ligi hiyo kwa kuwa na point 66 ikifuatiwa na Tottenham Hotspurs yenye point 61.

Picha ya kwanza kwa Hisani ya Soka360.com

Kama ulikosa kutazama goli la Taifa Stars lililofungwa na Samatta katika mchezo wa kwanza dhidi ya Chad

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andikaAYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments