Habari za Mastaa

Adele anaitambulisha rasmi official video ya mdundo wake mpya; “Hello” – (Video)!

on

Baada ya ukimya wa miaka minne msanii wa muziki wa Pop, Uingereza, Adele anaziandika headlines kwenye kurasa za burudani. Imepita miaka 4 toka adele aachie album yake ya mwisho iliyopewa jina 21, na kama wewe ni shabiki mkubwa wa Adele basi ipokee hii good news mtu wangu… Single ya kwanza kutoka kwenye album mpya ya Adele ipo hewani tayari!

ele1

Wimbo unaitwa ‘Hello’, video director si mwingine bali ni Director Xavier Dolan maarufu kama ‘Director X’. Album ya tatu ya Adele iliyopewa jina 25 itakuwa sokoni tarehe 20 November 2015 ikiwa imebeba nyimbo 11.

Kama bado hujakutana na single mpya ya Adele, basi karibu uitazame hapa chini kwa mara ya kwanza.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments