Leo July 13 2017 Katibu Mkuu ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Laurean Ndumbalo amezungumza na waandishi wa habari kuhusu watumishi wa umma ambao hawajawasilisha vyeti vyao vya kufaulu mtihani wa kidato cha nne na kidato cha sita kwa ajili ya kuahakikiwa na baraza la mitihani Tanzania.
Ndumbalo ameeleza kuwa watumishi ambao miundo ya maendeleo ya utumishi wao iliwataka kuwa na sifa ya kufaulu mtihani wa kidato cha nne wakati wanaajiriwa na ambao hawajawasilisha vyeti vyao kwa ajili ya kuhakikiwa na baraza la mitihani la Tanzania mishahara yao imesimamishwa kuanzia mwezi July 2017 hadi watakapowasilishavyeti hivyo. Bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Teknolojia ya Panya kutoka Tanzania ambayo inashinda za wazungu, Bonyeza play hapa chini kutazama