Kamisheni ya Haki za Binadamu Saudi Arabia imesema Serikali ya Taifa hilo imepiga marufuku adhabu ya vifo kwa Watoto ikiwa ni muendelezo wa hatua mpya za mabadiliko zinazotekelezwa na Utawala wa Kifalme wa Taifa hilo.
Hatua hiyo inachukuliwa, ikiwa imepita siku moja tu, baada ya kufutwa kwa adhabu ya kuchapwa viboko, Kamisheni hiyo inasema hakuna Mtoto atakaekutwa na hatia kisha akapewa adhabu ya kifo, badala yake atatumikia kifungo kisichopindukia miaka 10 katika Gereza la Watoto. •
Shirika la Kimataifa la Utetezi wa Haki za Binadamu la Amnesty International limeiweka Saudi Arabia katika orodha ya miongoni mwa Mataifa yanayonyonga Watu wengi zaidi, baada ya Iran na China na katika ripoti yake ya hivi karibuni kwa mwaka 2019 inaonesha Taifa hilo limewanyonga watu 184. ( via @dw_kiswahili )