Waziri wa zamani Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja leo July 10 ametangaza kurejesha pesa Tsh. milioni 40.4 za mgao kutoka kwa mfanyabiashara James Rugemalila ambaye inaelezwa alilipwa zaidi ya Bilioni 300 za ESCROW.
#MillardAyoBREAKING Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Sengerema CCM, William Ngeleja ametangaza kurejesha pesa za ESCROW. pic.twitter.com/v8kvPbO0JI
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
Ngeleja amesema alipokea msaada huo kama ilivyo kwa wabunge wengina bila kujua kama Rugemalila angekuja kuhusishwa na sakata la rushwa ya malipo ya ESCROW yaliyokuwa na utata mkubwa kati yake na serikali.
'Mimi nilipokea msaada ule kwa nia njema kama Wabunge wengine bila kujua James Rugemalila angehusishwa na kashfa za rushwa- @williamngeleja pic.twitter.com/VuzcjP3PpO
— millardayo (@millardayo) July 10, 2017
VIDEO: Umepitwa na hii ya Mtanzania aliyekataa mshahara wa milioni 425 Marekani? Bonyeza play kutazama hapa chini.