Michezo

Adil Rami akiri kupenda kula kumemponza

on

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa anayeichezea club ya Boavista ya Ureno kwa sasa Adil Remi (34) amesema angekuwa mchezaji mzuri zaidi wa soka kama angezingatia taratibu za chakula lakini alikuwa anapenda kula mno.

“Ningekuwa na maisha mazuri sana ya soka kama ningekuwa na lifestyle nzuri, kupenda mitoko, kuwa na wasichana wengi sikuzingatia kabisa suala la uzito wangu, tatizo langu kubwa ni chakula napenda kula sana”>>> Adil Rami

Kama utakuwa unakumbuka vizuri November 2016 katika exclusive interview ya @ayotv_ na Mbwana Samatta  kutokea Zimbabwe  alieleza kuwa mchezaji soka Ulaya unapangiwa chakula cha kula baada ya kupimwa, huli tu hukipendacho.

Samatta aliweka wazi kuwa yeye alishauriwa na Dr wake kutumia tambi zaidi (Spaghetti) tena za kumchemsha tu bila kuweka chochote.

Soma na hizi

Tupia Comments