Michezo

Adnan Januzaj ameondoka rasmi Manchester United

on

Masaa kadhaa kabla ya dirisha la usajili kufungwa barani ulaya, klabu ya Manchester United imeendelea kufanya biashara katika siku ya mwisho.

  
Baada ya jana kumpeleka kwa mkopo Tyler Blackett kwenda Celtic, Jonny Evans kwenda West Brom, leo hii imethibitishwa Adnan Januzaj amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Dortmund ya Ujerumani.

  Januzaj amekabidhiwa jezi namba 9 ambayo ilikuwa ikivaliwa na mshambuliaji Robert Lewandoski.

Wakati huo huo Manchester United leo imefanyia vipimo vya afya Mshambuliaji Anthony Martial kutoka klabu ya As Monaco ya Ufaransa.

Tupia Comments