AyoTV

VIDEO: Mabingwa wa Afrika wametua DSM, kocha kataja sababu ya kumuacha mchezaji bora Afrika

on

Mabingwa wa Afrika Mamelod Sundowns leo January 30 wamewasili Tanzania kwa ajili ya maandalizi yao ya kujiweka sawa katika mashindano tofauti tofauti, ikiwemo mchezo wa Super Cup dhidi ya TP Mazembe, Mamelod wamewasili Dar es salaam na msafara wa watu 42.
 
Kocha wao Pitso Mosimane ikabidi aulizwe kwanini hawajaja na mastaa wao golikipa Denis Onyango ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa Ligi za ndani na Khama Biliat, vipi wamekuja Tanzania wanampango wa kumchukua mchezaji yoyote kutokea Tanzania?
Khama na Onyango wangependa kuwepo lakini tumewapa mapumziko kwa sababu walikuwa AFCON wakati sisi tupo mapumziko, halafu tumecheza soka katika kipindi cha miezi 17 bila kupumzika hivyo kama wasipopata siku kadhaa za kupumzika inaweza kuwa hatari kwao kwa siku za usoni
“Mchezaji ni nanae weza kumuhitaji ni huyu mshambuliaji wenu aliyepo Ubelgiji Samatta ni kitu kizuri kuwa nae, lakini najua hayupo hapa kwa sasa, lakini tutaangalia pia hapa Tanzania kwa sababu hii ni sehemu ya kujenga kikosi chetu najua tutacheza na Yanga, Azam FC na Simba hizi ni timu nzuri na imara pia”

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments