April 7 kila mwaka Dunia huadhimisha Siku ya Afya ambapo leo ni April 7, 2017 nimeona siyo vibaya nikikusogezea list ya nchi 25 zenye wananchi wenye afya nzuri zaidi duniani.
Katika kuadhimisha Siku ya Afya Duniani 2017, Bloomberg Health Index imeziorodhesha nchi 25 zenye wananchi waliokuwa na afya nzuri ambapo Italia imetajwa kama kinara kwa kuwa na wananchi wenye afya na wanaoishi kwa miaka mingi hadi kufikia miaka 100.
Sierra Leone imetajwa pia kuwa miongoni mwa nchi zenye wananchi wasio na afya duniani na kwa mujibu wa list hii nchi zilizotajwa zinaongoza kwa kuwa na asilimia chache ya vifo kwa mwaka huku zikiwa na hospitali za kutosha, asilimia ndogo ya magonjwa ya kuambukiza na wananchi wake huishi miaka mingi ukilinganisha na nchi nyingine.
VIDEO: Ulipitwa na hii ya Wizara ya Afya kuhusu ugonjwa wa ZIKA? Bonyeza play kutazama.
BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo