Mtu mmoja anayefahamika kwa jina Mbaruku mussa anayekadiriwa kuwa na miaka 47 makazi wa mtaa wa olmoti kata ya olimoti mkoani Arusha anahofiwa kufariki baada ya kudaiwa kupewa Dau la fedha shilingi elfu arobaini (40) kuingia katika kisima cha maji chenye mita zaidi ya 60 kwenda kumtoa mbuzi aliyedumbukia humo.
Viongozi pamoja na wananchi wanadia kuwa wameweka kambi kwa siku ya tatu hadi hii leo wakiwa na askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji kwa ajili ya kuokoa lakini hadi hii leo imeshindikana
“Walikuja vijana watano ambao walizama kwenye shimo kwa shilingi elfu arobaini lakini baadaye ilitokea kishindo katika kisima yule bwana kuchungulia tukakuta ameshadumbukia kwenye kisima nikawaambia wavute kamba ikarudi yenyewe,walikubaliana watamtoa huyo mbuzi kwa elfu 40 ndio wakazama kwenye kisima,baada ya tukio wengine wakakimbia”Chacha Joseph -Shuhuda
Kwa upande wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Arusha wamefika eneo la tukio na kuendelea na jitihada za uokozi lakini hadi Ayo Tv inaondoka eneo la tukio hawakuweza kufanikiwa