Timu ya taifa ya Tanzania yenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys bado ipo nchini Gabon katika mji wa Libreville kunakochezwa michezo ya Kundi B ya AFCON U-17,Serengeti Boys imepangwa Kundi B na timu za Angola, Mali na Niger.
Kesho Serengeti Boys watacheza mchezo wao wa pili dhidi ya Angola lakini kama ufahamu shirikisho la soka la Afrika CAF limetoa ulinzi kwa timu shiriki ikiwemo na escort ya polisi wakiwa wanaenda na kurudi uwanjani sambamba.
Serengeti Boys wamepewa walinzi zaidi ya 10 ambao wanatembea nao katika msafara wao wakiwa mazoezini au hata hotelini, basi la Serengeti Boys wanaoruhusiwa kupanda ni wachezaji na benchi la ufundi pekee.
Kingine kinachoweza kukushangaza au kukuvutia ni kuwa CAF wanajali timu shiriki za michuano hii, msafara wa Serengeti Boys huwa na magari yasio pungua manne, kuna basi la wachezaji, ambulace ambayo pia inashinda katika hoteli ya wachezaji, gari mbili za walinzi na gari la viongozi ambao watakuwa wameongozana na timu.
VIDEO: Alichoamua Rais wa Simba baada ya kupokwa point 3 na TFF vs Kagera