Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Jumanne Muliro amesema pamoja na watuhumiwa mbalimbali waliokamatwa na Jeshi hilo kwa makosa ya wizi pia, limemkamata na linamuhoji kwa kina Hassan Chambilia Sumilanda (28) maarufu kama ‘Dkt. Hassan Mangena, mkazi Sinza Kumekucha, kwa tuhuma za kujipatia pesa kwa njia ya udangayifu kwa kudai kuwasaidia watu kupata kazi au uhamisho jambo ambalo sio la kweli.
Inadaiwa, Mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia hafla za kiserikali kupiga picha na viongozi wakubwa wa Serikali na kuziweka katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii kwa jiina la Hassani Mangena na kujitambulisha kuwa ni mtumishi wa Serikali kutoka Wizara ya afya kitengo cha mama na mtoto, wakati mwingine hujitambulisha kuwa ni Kaimu Mkurugenzi wa idara ya afya Ustawi wa jamii na lishe na kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Kamanda Muliro amesema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo kwa hatua zaidi za kisheria.