Maelfu ya watu kutoka Deir Al-Balah katikati mwa Ukanda wa Gaza wameshiriki katika mazishi ya afisa mkuu katika tawi la kijeshi la Hamas, Brigedi za Al-Qassam. Kifo cha Ghazi Abu Tama’a kilitangazwa rasmi siku chache zilizopita.
Msemaji wa Brigedi za Al-Qassam, Abu Obeida, alithibitisha kuwa kamanda wao mkuu, Mohammad Al-Deif, aliuawa pamoja na maafisa wengine wakuu, akiwemo Abu Tama’a.
Ghazi Abu Tama’a, anayejulikana kama “Abu Musa”, alikuwa Kamanda wa Sehemu ya Huduma za Silaha na Mapambano hadi kifo chake, na mjumbe wa baraza la kijeshi la Brigedi.
Jeshi linalokalia kwa mabavu lilitangaza mauaji yake pamoja na Marwan Issa mwezi Machi mwaka jana katikati mwa Ukanda wa Gaza.