Mwanajeshi mkongwe wa CIA alishtakiwa Jumatatu kwa kuuza siri za Marekani kwa China kisha bila kufahamu kukubali ujasusi wake kwa FBI huku waendesha mashtaka wakisema walitumia kumfanya afichue asili ya ujasusi wake na ilistahili kuwa riwaya ya kijasusi yenyewe.
Alexander Yuk Ching Ma, 71, alikamatwa mnamo Agosti 2020 baada ya kukiri kwa ofisa wa kisiri wa Shirika la Ujasusi la Marekani (FBI) kwamba aliuza siri za Marekani kwa China.
Ma, raia wa Marekani aliyezaliwa Hong Kong, alifanya kazi katika shirika la ujasusi la CIA kutoka 1982 hadi 1989 baadaye alifanya kazi na shirika la FBI katika taaluma yake.
Sehemu ya makubaliano ya kukiri mashtaka inasema kwamba lazima ashirikiane na waendesha mashtaka “katika maisha yake yote, ikiwa ni pamoja na kujiwasilisha akihitajika kuhojiwa na mashirika ya serikali ya Marekani”.
Makubaliano hayo yanamtaka kujiwasilisha katika vipimo vya mashine iliyoundwa kutambua na kurekodi mabadiliko katika sifa za kisaikolojia, kama vile mapigo ya moyo na viwango vya kupumua vya mtu, vinavyotumiwa hasa kama kitambua uwongo maarufu kama ‘polygraph’, kulingana na shirika la habari la Associated Press.
Katika kusikilizwa kwa hukumu siku ya Jumatano, mawakili wa serikali ya Marekani waliiambia mahakama kwamba amekuwa akitoa ushirikiano, na tayari ameshiriki katika “vikao vingi vya mahojiano na mashirika ya serikali”.
Alipokuwa akiishi Hawaii mwaka wa 2004 alipata kazi katika ofisi ya FBI ya Honolulu kama mwanaisimu wa mkataba.