Duniani

Watumiaji wa simu Afrika ni wengi kuliko wanaopata maji salama ?? Umeme, barabara je?

on

Ishu kwenye healines inagusa Afrika ambapo ripoti ya utafiti wa Afrobarometer, ni ripoti ambayo CNN wameipandisha kwenye mtandao wao January 19 2016, ina majibu kuhusu ishu ya watu ambao wanapata huduma ya majisafi, wenye mawasiliano ya simu za mkononi, umeme na mengine.

Majibu ya ripoti hiyo yanaonesha watu wanaotumia huduma ya simu za mkononi ni 93% ya watu wote waliopo Afrika, wakati huohuo watu wanaopata huduma ya majisafi ni 63%.

AFROBAROMETER

Kwenye ripoti hiyo majibu mengine yapo pia kwamba watu wa Afrika, 65% wanapata huduma ya umeme, 54% wanatumia barabara zinazopitika, na 30% tu ndio wanaoishi kwenye makazi ambayo yana huduma ya kuhifadhi majitaka.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments