Duniani

Rekodi nane kubwa kwa leo >> kiboko wauaji, tembo wa Africa, treni kali Africa na mengine.. (+Picha)

on

Nimekutana na ripoti kwenye channel ya ETV ya South Africa ambayo imegusa vitu mbalimbali… kati ya simba na mnyama kiboko, yupi anaongoza kwa kuua binadamu ??!! Jibu lake ninalo hapa pamoja na mengine mengi mtu wangu.

IMAG1855

Unaambiwa japo Kenya ni moja ya nchi wazalishaji wakubwa wa kahawa ambayo inauzwa nje ya nchi, Wakenya wenyewe wanapendelea zaidi chai na bia.

IMAG1857

Kope za jicho la binadamu zinacheza kwa wastani wa mara milioni 4.2 kwa mwaka… umeipata hiyo ??!!

IMAG1859

Seli za kwenye ubongo wa binadamu ndio seli zinazoishi kwa muda mrefu zaidi kuliko nyingine zozote, na zinaweza kuwa hai kwa kipindi chote cha uhai wa binadamu.

IMAG1861

Jangwa la Sahara lililopo kaskazini mwa Afrika ndio jangwa kubwa zaidi kuliko majangwa yote duniani.

IMAG1864

Treni la Rovos Rail lililopo South Africa ndio treni la kifahari zaidi duniani.

IMAG1866

Ulijua hii mtu wangu ?! Kumbe mnyama kiboko anaua watu wengi zaidi kuliko simba.

IMAG1872

Unaambiwa tembo wanaopatikana Africa ndio mnyama mkubwa zaidi anayeishi ardhini duniani.

IMAG1873

Mto Nile unaoanzia Ziwa Victoria upande wa Uganda na kuishia Misri ndio mto mrefu zaidi duniani.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments