Raia nchini Afrika Kusini wametakiwa kuchukua tahadhari baada ya mamlaka kwenye taifa hilo kuthibitisha visa viwili vya ugonjwa wa kipindupindu kaskazini mwa wilaya ya Limpopo.
Kulingana na idara ya afya katika wilaya hiyo imesema kuwa wagonjwa wote wawili ni raia wa Zimbabwe walioingia kwenye hilo kupitia maeneo ya mpakani.
Aidha idara hiyo ya afya imeeleza kuwa kisa cha kwanza kilithibitishwa baada ya mgonjwa mwenye umri wa miaka 43 kupatikana na maambukizi hayo baada ya kufanyiwa vipimo.
Kisa cha pili kilikuwa cha mwanaume mwengine mwenye umri wa miaka 27 ambao wote kwa sasa wametengwa hosipitalini.
Mamlaka imeeleza kuwa visa vyote viwili vilitokea nchini Zimbabwe, taifa ambalo linakabiliwa na msambao wa kipindupindu.