Mix

Afrika Kusini kwenye headlines tena na mabadiliko ya Sheria!

on

SA

Ulikuwa unafahamu ya kuwa kuna baadhi ya nchi za Kiafrika haziruhushu vijana chini ya umri wa miaka 18 kufanya mapenzi? Na adhabu yake mtu akikamatwa ni kifungo!?

Nimekutana na stori kutoka South Africa inayoweka headlines usiku wa leo, South Africa hapo awali ilikuwa na Sheria iitwayo Sheria ya Makosa ya Jinai (Makosa ya Kujamiana na Mashirika Mamo) iliyokuwa inakataza vijana chini wa miaka 18 kufanya mapenzi.

cover

Mwezi uliyopita Serikali ya South Africa ilifanya mabadiliko ya Sheria hiyo na Mwenyekiti wa Kamati Kwingineko juu ya Haki na Huduma za Magereza Mathole Motshekga alisema hapo awali aliamini kuwa kama jamii jukumu lao ni kuwafundisha watoto kujichunga,  lakini alikuwa anakosea na kuwanyima watu hao haki zao za kibinadamu.

MATHO

Mathole Motshekga

 Bunge la Katiba lilikaa na kufanya mabadiliko juu ya vifungu 15 na 16 ya Sheria hiyo kwa kusema kuwa Vifungu hivyo vinaenda kinyume na Katiba inayosema kila Raia ana uhuru wa maamzi yake binafsi na pia ni kinyume na haki za binadamu.

south-africa-parliament

Bunge la Katiba limesema kila mtu iwe mkubwa au mdogo ana haki ya kufanya maamuzi binafsi yanayomhusu yeye bila kupingwa au kuingiliwa na mtu yoyote.

 Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments