Habari za Mastaa

MAHAKAMANI: Mkojo wa Agness Masogange wakutwa na chembechembe za dawa za kulevya

on

Kutoka kwenye Mahakama ya hakimu mkasi Kisutu Dar es salaam leo kwenye kesi inayoendelea ya Mrembo Agness Gerald maarufu kama Agness “Masogange” Mkemia kutoka Ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali amesema mkojo wa Agness umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya.

Mkemia Elias Mulima (40) ameiambia Mahakama kwamba mkojo wa Agness umekutwa na chembechembe za dawa za kulevya aina ya heroine na oxazepam na heroine (Diacety Imophine).

Amesema sampuli ya mkojo wa Agness zilizowasilishwa kwao zilikua na chembechembe za dawa za kulevya ambapo Mulima ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya Masogange kukutwa na dawa za kulevya Februari 15 2017 Dar es salaam, alidai hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Agness Masogange Mahakamani leo Aug 2 2017

Akiongozwa na Wakili wa Serikali Constantine Kakula.. Shahidi huyo alidai kuwa Februari 15 mwaka huu katika ofisi ya Mkemia mkuu Dar es salaam akiwa ofisini alipokea vielelezo kutoka Jeshi la Polisi vilivyowasilishwa na koplo Sospeter na WP Judith kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ili kubaini kuwa ni dawa za kulevya au la.

Shahidi huyo alidai kuwa iliwasilishwa na fomu maalumu ya dawa za kulevya ambayo ilikua na namba DCEA 008 na alifanya usajili na kuipa namba ya maabara 446/2017 ambapo Mshtakiwa alipewa kontena maalumu kwa ajili ya sampuli ya mkojo.

Aliandaa taarifa ya uchunguzi iliyosainiwa na kuthibitishwa na Kaimu mkemia Mkuu wa Serikali inayoonesha madhara ya mtumiaji kuwa na ulevi usiotibika pamoja na kuharibikiwa kiakili ambapo
Shahidi huyo aliomba Mahakama kupokea vielelezo hivyo ambavyo ni fomu maalumu za uchunguzi wa sampuli hiyo na kusema anavitambua kwa saini yake, muhuri wa moto na jina la Mshitakiwa.

Upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Nehemia Nkoko ulipinga ukidai kuwa fomu hizo hazijakamilika hivyo haziwezi kupokelewa kama kielelezo ikiwa ni sehemu ya ushahidi na kuiomba Mahakama ipuuze.

Wakili wa Serikali kakula alidai mapingamizi hayo hayana mashiko kwa sababu fomu hizo zina utofauti hivyo kuiomba Mahakama kupokea vielelezo hivyo ambapo Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28 mwaka huu kwa ajili ya kupitia vielelezo hivyo.

KWANINI WEMA SEPETU HAJAKABIDHIWA KADI YA CHADEMA JANA? PLAY HAPA CHINI KUFAHAMU

MSIBA HARUSINI: Bibi Harusi kafariki saa 11 baada ya kuolewa, play hapa chini kupata taarifa kamili

VIDEO: EBIITOKE AFUNGUKA……. “BEN POL HAJANILIPA”

Soma na hizi

Tupia Comments