AyoTV

Maamuzi ya Mahakama kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM (+Video)

on

December 19, 2017 Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma imetoa dhamana kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mbunge wa Donge, Zanzibar Sadifa Juma Khamis anayetuhumiwa kwa kesi ya rushwa.

Sadifa Juma Khamis alikamatwa nyumbani kwake Dodoma December 9, 2017 kwa tuhuma za Rushwa akidaiwa kuwapa wajumbe kutoka Kagera vinywaji na pia kuahidi kuwalipia nauli ili wamchague Mwenyekiti mpya wa UVCCM aliyekuwa akimpigia kampeni.

Wakili wake Godfrey Wasonga amefanyiwa EXCLUSIVE INTERVIEW na Ayo TV nje ya Mahakama na kusema “Mahakama imeamua kumpatia dhamana Sadifa Juma Khamis baada ya kujiridhisha kwamba hakuna shaka kwa mujibu wa sheria inayomzuia dhamana hivyo amepewa dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili kila mmoja akiwa na bondi ya milioni moja”

HOTUBA YA JPM KATIKA MKUTANO MKUU WA CCM DODOMA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments