Michezo

Aguero agawa Range Rover yake Man City

on

Mshambuliaji wa zamani wa Man City raia wa Argentina aliyejiunga na FC Barcelona hivi karibuni Sergio Aguero ameondoka Man City kwa kugawa zawadi kwa staff wa timu hiyo ambao amefanya nao kazi kwa miaka 10.

Aguero kabla ya kuondoka aliamua kuchezesha bahati nasibu kwa staff wa Man City nani atamuachia Range Rover yake inayotajwa kuwa na thamani ya Pound 40,000 (Tsh milioni 130).

Bahati nasibu hiyo imefanyika na mshindi akapatikana lakini amewanunulia saa staff wote kama zawadi yake kwa kuishi nao vizuri.

Aguero ametajwa kununua saa 60 za brand ya Hublot au Tag Heuer ikitajwa kila moja kuwa na thamani isiyopungua pound 1000 (Tsh milioni 3.2).

Soma na hizi

Tupia Comments