Ligi Kuu England imeendelea tena leo lakini kwa kushuhudia Mabingwa watetezi Man City wakiwa wageni wa Aston Villa, game hiyo imemalizika kwa mshambuliaji wa Argentina na Man City Sergio Aguero kuandika rekodi mpya EPL.
Baada ya kufunga hat-trick dhidi ya Aston Villa katika ushindi wa 6-1 wa Man City, Sergio Aguero ameandika rekodi ya kuwa mchezaji pekee katika historia ya EPL kuwahi kufunga hat-trick 12.
Sasa Aguero anakuwa kavunja rekodi ya Alan Shearer ambaye kwa sasa amekuwa ni kama anafuatiwa Aguero, Alan Shearer mwenye hat-trick 11 aliyoiweka rekodi hiyo 1999 kwa sasa amestaafu soka toka 2006 na hana tena nafasi ya kupindua rekodi ya Aguero.