Top Stories

Kesi ya Bil.2 inayomkabili Mkurugenzi wa UDART imefutwa kwa sababu hizi (+video)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu imemfutia mashtaka aliyekuwa Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART) Robert Kisena na wenzake watatu.

Kisena na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka 19 ikiwemo la utakatishaji wa fedha na kuusababishia Mradi wa UDART hasara ya zaidi ya Bil 2.41.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kulwa Kisena, Charles Newe na raia wa China, Cheni Shi.

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu 91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai(CPA),sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokuwa hana nia ya kuendelea na kesi hiyo.

MASIKINI !! FAMILIA HII IMEKWENDA GEREZANI, INADAIWA KUSABABISHA HASARA YA BIL.2

Soma na hizi

Tupia Comments