Habari za Mastaa

Cardi B aahirisha tamasha lake kisa upasuaji

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Cardi B amejitoa kutumbuiza kwenye tamasha la 92Q Spring Bling Ijumaa hii mjini Maryland kutokana na kupata tatizo baada ya upasuaji wa kutengeneza mwili (liposuction) alioufanya baada ya kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na rapper huyo vimeeleza kuwa kwa sasa yupo kwenye mchakato wa kupona baada ya kufanya pia upasuaji wa maziwa yake na madaktari wameshauri kuwa Cardi B anahitaji mapumziko ya muda mrefu ili mwili wake urudi kama zamani kutokana na baadhi ya sehemu alizofanyiwa upasuaji.

Inaelezwa kuwa Cardi B alifanya upasuaji huo baada ya kubahatika kumpata mtoto wake wa kwanza Kulture, imeelezwa pia May 5,2019 Cardi B alisikika akiwaambia mashabiki zake katika tamasha lilofanyika Memphis kuwa alitaka kuahirisha tamasha hilo kwasababu kucheza sana kunaweza kumsababishia matatizo.

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA MOSE IYOBO KUTOTOKEA KWENYE BIRTHDAY YA MWANAE, AUNT EZEKIEL KAZUNGUMZA?, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Soma na hizi

Tupia Comments