Michezo

Unajua PSG wamepewa ahadi ya kiasi gani ikiwa wataitoa Chelsea leo usiku

on

PSG-vs-CHEYakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya mchezo wa pili wa hatua ya robo fainali ya Champions league kati ya Chelsea dhidi ya PSG, Raisi wa klabu ya PSG Nasser Al-Khelaifi ametoa ofa nzito kwa wachezaji wa klabu hiyo endapo watafanikiwa kuitoa Chelsea leo hii.

PSG ambao waliifunga Chelsea 3-1 wiki iliyopita jijini Paris wana nafasi ya kusonga mbele kutokana na ushindi walionao mkononi lakini katika kuhakikisha timu yake inafanya vizuri Al-Khelaifi ametoa ofa ya kiasi cha €450,000 ni zaidi ya billioni 1 kwa fedha za madafu, kwa kila mchezaji wa PSG endapo klabu hiyo itafanikiwa kuingia nusu fainali.

Hatua inakuja siku chache baada ya kutoa ahadi ya €400,000 kwa kila mchezaji ikiwa tu watatetea kombe la ligue 1.

Tupia Comments