Mwanamke mmoja huko Indiana, Blossum Kirby, hivi majuzi alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kuwabeba watoto wake mapacha wa miezi [2] kwenye sanduku akiendesha baiskeli kuzunguka jiji hilo huku watoto hao wakilia.
Kisa hicho kilionekana wakati wafanyikazi kutoka duka moja la kuuza pizza walipomwona mwanamke huyo akiwazungusha watotot hao bila hata mwamvuli ndani ya kreti la plastiki lililounganishwa mbele ya baiskeli hiyo.
Watoto hao walikuwa wamevaa nepi pekee, wamechomwa na jua, na walikuwa na majeraha madogo hiyo ni baada ya uchunguzi,na Kirby alipatikana na hatia ya kutelekeza watoto na kushtakiwa kwa makosa mawili ya utelekezaji wa watoto na alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa matendo yake.
Tukio hilo limezua hasira na mjadala kuhusu usalama wa watoto na wajibu wa wazazi linapokuja suala la ustawi wao huku baadhi ya watu wakimkosoa Kirby kwa vitendo vyake, wengine wameonyesha huruma kwake, wakitaja kuwa huenda amekuwa akipitia wakati mgumu na huenda hakupata njia nyingine ya usafiri.
Utelekezaji wa watoto ni suala zito huko Indiana, huku viwango vya unyanyasaji vikiwa juu zaidi ya wastani wa kitaifa na kulingana na takwimu za unyanyasaji wa Mtoto na Kutelekezwa huko Indiana, kutelekezwa kulichangia 71% ya visa vyote vilivyoripotiwa, na watoto wa miaka mitatu au chini ndio walio hatarini zaidi.