Arobaini za mwanamume mmoja nchini Nigeria, zilifika baada ya kunaswa akiwaibia waumini kanisani katika jimbo la Lagos na kukutwa akificha mali hizo zote katika choo cha kutumia maji kanisani hapo.
Mwanamume huyo aliyefahamika kama Ebuka Iheanacho, anaonyeshwa kwenye video akihojiwa na waumini wa kanisa hilo ambao walimfumania.
Baada ya kubanwa na maswali ya waumini hao, Ebuka aliungama dhambi zake akifichua kuwa mama yake pia huenda katika kanisa hilo kama omba omba.
Ilibainika kuwa jamaa huyo alikuwa akificha vitu alivyoiba katika choo cha kanisa hilo na siku hiyo ambayo alinaswa, alikuwa ameiba simu kadhaa na begi.
Julai 2, 2021, mwanamke ambaye ni mama wa kijana huyo anaonyeshwa akiwa ndani ya chumba kimoja na kikapu cha sadaka kisha alichukuwa pesa alizohitaji na kuingiza ndani ya sidiria yake na baada ya kuhisi ameridhika na kiasi hicho cha pesa, aliondoka haraka kwenye chumba hicho kabla ya kukamatwa.
Hali za wizi katika nyumba za ibada zinatafsiriwa na wataalamu wa masuala ya kiuchumi kuwa ni kutokana na ugumu wa maisha lakini viongozi wa dini wakisema kuwa ni katika hali ya kutomuogopa Muumba.