Mwanamume kutoka Tennessee Joseph Braswell (36) ameripotiwa kukamatwa baada ya kula mifuko miwili ya chipsi zilizoibiwa na mtu mwingine kutoka kwenye duka la bidhaa na kutelekezwa nje kidogo ya duka hilo.
Kwa mujibu wa WREG, tukio hilo lilijiri katika duka la Circle K lililopo katika kijiji cha Parkway, Memphis, mapema mwezi huu, wakati mwanamume mmoja alipoingia kwenye mzozo na muuzaji wa duka hilo ambaye alikataa kumuuzia pombe yoyote.
Kwa kulipiza kisasi, mwanamume huyo aliamua kuchukua sanduku lote lililojaa takriban mifuko mia moja ya chips alipokuwa akitoka dukani na kuzitelekeza nje ya gari lake ndipo bwana braswell alipoziona nakuanza kuzishambulia!
Braswell alikaa gerezani kwa siku kadhaa kabla ya kuachiliwa, lakini mama yake amezungumzajuu ya kukamatwa kwake, akisema kwamba amekuwa akijaribu kumpima kwa daktari wa akili kwa muda, akionyesha kuwa Braswell anaweza kuwa na shida za afya ya akili.
Si mara ya kwanza kwa bwana braswell kufanya matukio kama haya kwani baadhi ya makosa yake ya awali yanasemekana kuwa ni pamoja na kuendesha gari bila leseni, ukiukaji wa muda wa majaribio, na matukio ya kushambuliwa nyumbani.