Tulianza kumfahamu Aika kwenye bongofleva kupitia kundi la Pah One lakini baadae wakaanzisha kundi jipya la Navy Kenzo ambalo wako yeye na mpenzi wake ambaye ni producer pia Nahreel.
Nyota njema ilikuwa upande wao, wakafanya poa na singlee zao kama Moyoni, I Just Wanna Love You, Chelewa, Aiyola na nyingine nyingi mtu wangu..
Leo millardayo.com imekusogezea exclusive ya msanii Aika ambaye kama ulikua hujui ilibaki nusu arudi kwao Arusha na aachane na muziki kwa muda, na haya maamuzi yangefanyika siku chache sana kabla ya kutoa hit single ya chelewa.
Aika amesema kabla ya kuachia hiyo single walikutana na changamoto nyingi ikiwemo kukosa studio na kama muziki wao kutokukubalika ndio maana wakaona ni bora wafanye kitu kingine kusukuma maisha na sio muziki tena.
So angerudi nyumbani kwao Arusha na kumuacha Naareel? kwenye hii sentensi anasema >>> “kuna maamuzi kwenye maisha unafanya bila kuangalia vipi inakuwaje.. mimi na Nahreel tunafanya kila kitu pamoja, may be tungeenda wote yani tulikuwa kwenye hiyo stage, sijui labda tungeenda wote… tulianza kufanya muziki 2011 tulivyorudi kutoka India “
Bonyeza play hapa chini kumsikiliza Aika
millardayo.com ndio sehemu utakayozipata story zote mtu wangu, unaweza kuwa karibu zaidi na mimi kwa kujiunga kwenye Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook