Michezo

Azam FC imemrudisha Aristica Cioaba bye bye Ndairagije

on

Kocha mkuu wa Azam FC Etienne Ndairagije ni wazi sasa anaelekea kutangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars baada ya kuwa kaimu kochi wa Taifa Stars katika mechi 7.

Imeripotiwa kuwa baada ya Etienne Ndairagije kuwa kaimu kocha mkuu wa Taifa Stars kwa mechi saba sasa huku akiiwezesha Taifa Stars kufuzu kucheza CHAN 2020 na makundi ya kuamua kufuzu World Cup 2022, wameamua kumpa mkataba.

Hivyo Azam FC wameamua kutafuta mbadala wake ambaye ni Aristica Cioba kutoka Romania aliyewahi kuifundisha timu hiyo kwa muda mfupi miaka miwili iliyopita, Ndairagije ameaga rasmi Azam FC na wakati wowote kutokea sasa atatangazwa kama kocha mkuu wa timu hiyo.

Soma na hizi

Tupia Comments