Matukio ya ajali za ndege yameendelea kuchukua headlines katika vyombo mbalimbali vya habari duniani.
Ikiwa ni siku chache baada ya ndege ya Urusi kuanguka na kuua zaidi ya watu 200 huko Sinai, Misri taarifa nyingine iliyotufikia muda mfupi uliopita ni wa hii ajali nyingine iliyotokea Sudan Kusini na kuua watu 41.
Ndege hiyo mali ya Serikali ya Russia ambayo ni maalum kwa kubeba mizigo ilikua na abiria wachache huku ikidaiwa kuangukia watu ardhini na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 41.
Ndege ilikuwa ikitokea uwanja wa ndege wa Juba kuelekea mji wa Paloch katika jimbo la Upper Nile na ilianguka kwenye ukingo wa Mto Nile.
Maafisa wa uwanja wa ndege wamesema mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo pamoja na mtoto mdogo ndio waliweza kunusurika.
Airplane just crashed near Juba Int’l Airport shortly after taking off. #EyeRadio’s D Santo: over 40 passengers died pic.twitter.com/SuFExWfX0Z
— Eye Radio Juba (@EyeRadioJuba) November 4, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFB YOUTUBE.