Duniani

Ndege zimetelekezwa airport mwaka mzima, mwenye nazo hajulikani ?!! Cheki na hii ya ndege tatu..

on

Eti ndege zimetelekezwa na mwenyewe hafahamiki ??!! Kichwa cha habari huenda kikakushtua lakini ndio hivyo, na ndege zenyewe zimekaa airport mwaka mzima uwanja wa Kuala Lumpur, Malaysia.

Baada ya ndege hizo kutekelezwa uwanjani hapo kwa zaidi ya mwaka mmoja, ilibidi uongozi wa uwanja huo wapeleke matangazo magazetini kutaarifu kwamba kwa mmiliki wa ndege hizo ajitokeze kutoa ndege zake ndani ya siku 14, kama asipotokea basi ndege hizo zinauzwa !!

Hizi ni sehemu ya ndege hizo tatu zilizotelekezwa.

Hizo ni sehemu ya ndege hizo tatu zilizotelekezwa.

Baada ya tangazo hilo kutoka magazetini December 09 2015 na kuchukua headlines mitandaoni, taarifa nyingine iliyonifikia na kuripotiwa na mtandao wa Daily Mail ni kwamba Kampuni ya Swift Air Cargo imejitokeza na kusema wao ndio wamiliki wa ndege hizo tatu kubwa za mizigo…

SWIFT

Hili ndio tangazo la ndege hizo gazetini.

Uongozi wa uwanja huo bado wanaendelea na uchunguzi kujithibitishia kama kweli Swift Air Cargo ndio wamiliki halali wa ndege hizo… lakini cha kujiuliza ni kwamba, inakuwaje mpaka ndege zikasahaulika airiport kwa mwaka mzima ??!! Ndio headlines zenyewe duniani mtu wangu, watu wanasahau mpaka ndege !!

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments