Stori Pekee

Kwenye viwanja vya ndege vilivyotelekezwa, viko na hivi nane kwenye pichaz kabisa..

on

runway-man

Ukiangalia gharama za kujenga Viwanja vya Ndege huwezi amini kwamba kuna mahali kwingine Viwanja hivyo vimetelekezwa na havifanyi kazi kabisa japo gharama nyingi zimetumika kuvijenga!!

Kuna hivi hapa ambavyo vingi vina Historia ya kutumiwa na Vikosi vya Majeshi lakini baadae Kambi zimefungwa na kumebaki tu hakuna kinachoendelea.

PEARLS AIRPORT

Željava Air Base, hiki kilijengwa kwenye Milima ya Plješevica katikati ya miaka ya 1957 na 1965, kiligharimu kama Dola Bilioni 6 hivi kwa ajili ya shughuli za Kambi ya Jeshi la Yugoslavia, baadae mwaka 1991 wakaachana na Uwanja huo ambao waliweka Kambi yao mpaka sasahivi pametelekezwa na hakuna mwenye biashara napo tena !!

ELLINIKON INTERNATIONAL AIRPORT- GREECE

Hii ni Ellikon International Airport, ilijengwa mwaka 1938 Jiji la Athens Ugiriki.. lakini wakati wa Vita ya pili ya Dunia, Kikosi cha NAZI kilichoongozwa na Adolph Hitler wakati ule kilivamia hapa kabla hata ujenzi haujakamilika, baadae Serikali ya Ugiriki iliruhusu Vikosi vya Kijeshi viutumie Uwanja huu kwa shughuli zao. Mwaka 2001 nao waliutelekeza wakaondoka zao, kulikuwa na mpango wa Serikali ya Ugiriki kutenga Euro Bilioni 7 kupaendeleza lakini kutokana na hali ngumu ya Kiuchumi ya Ugiriki, mpaka sasahivi nyasi zimeota mpaka mlangoni, imebaki story tu !!

FLOYD BENNETT FIELD- BROOKLYN, N.Y.

Hapa ni Marekani, Kiwanja kiko kwenye Visiwa vya Barren, New York… Hiki kilikuwa Kiwanja cha kwanza cha Ndege cha Manispaa New York mwaka 1931. Hapa panaitwa Floyd Bennett Field, mwaka 1941 Uwanja uliuzwa kwa Kikosi cha US Navy, walivyopaacha na wenyewe sasahivi ni sehemu tu ambayo watu wanakatisha kuona vitu vilivyotelekezwa ikiwemo ndege za kivita na magari ya Kijeshi.

GAZA INTERNATIONAL AIRPORT- GAZA

Gaza International Airport ni Uwanja ambao uko Palestina, ulijengwa kwa Dola Milioni 86 na ulifunguliwa mwaka 1998, lakini miaka mitatu baadae Uwanja ulifungwa baada ya Radar ya kuongozea Ndege kupigwa mabomu na Vikosi vya Jeshi la Israel. Baadae ulibadilishwa jina na kuitwa Yasser Arafat International Airport, pamebaki tu kuwa sehemu ambayo ina majengo ya kumbukumbu.

JOHNSTON ATOLL AIRPORT

Muonekano wa Uwanja wa Ndege wa Johnston Atoll Airport, kwenye Visiwa vya Hawaii Marekani. Zamani ilikuwa ni Kambi ya Jeshi la Marekani kwa muda mrefu, na walipatumia pia kuhifadhi na kujaribia silaha za kijeshi… Mara chache sana Uwanja wa Ndege kwenye Kambi hii unatumiwa kama ikitokea dharura lakini hawana mpango napo tena toka 2005 Kambi ya Kijeshi ilivyofungwa.

MARINE AIR CORPS STATION EL TORO

Marine Air Corps Station, hapa ni California Marekani.. Palikuwa pakitumiwa na Kikosi cha Jeshi tangu mwaka 1943, baadae mwaka 1999 palitelekezwa na hakuna shughuli yoyote ya msingi inayofanywa hapa. Will Smith aliwahi kufanya sehemu ya Series za Top Gear kwenye eneo hili.

THE NICOSIA INTERNATIONAL AIRPORT- CYPRUS

Nicosia International Airport, uliwahi kuwa Uwanja mkubwa wa Ndege kwenye Visiwa vya Cyprus.. Uwanja ulifunguliwa mwaka 1939, baadae pakashambuliwa na Jeshi la Uturuki mwaka 1974, upande mmoja wa Uwanja unatumiwa na Vikosi vya Umoja wa Kimataifa vinavyohusika na kulinda amani, kwingine kumebaki hakuna kinachofanya kazi kwa zaidi ya miaka 40 sasahivi.

UPPER HEYFORD BASE- OXFORDSHIRE, ENGLAND

Upper Heyford Base, hili eneo liko Oxfordshire Uingereza… Hili eneo lilitumiwa na Vikosi vya Jeshi la Uingereza kuanzia mwaka 1918 mpaka 1950, baadae vikaweka Kambi Vikosi vya Jeshi la Marekani lakini nao waliondoka mwaka 1993. Sio sehemu ambayo mtu unaruhusiwa kukatisha kwa sasahivi, kuna ulinzi japo hapatumiwi tena.. Serikali ina mpango kupafanya eneo la Kumbukumbu.

Hii imekaa kihistoria zaidi yani, najua hata TZ kuna maeneo ukikatisha unakuta Majumba ya zamani yametelekezwa na yana historia zake pia… na kwa wenzetu yapo mtu wa nguvu !!

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments