Katika kurudisha kwa jamii kampuni ya ndege ya AirTanzania imetoa msaada wa meza na viti vyenye thamani ya milioni 70 katika shule ya sekondari Tanga ufundi ikiwa na lengo la kuhamasisha vijana wa kike kusoma masomo ya sayansi ili kuweza kuwa kuwa marubani.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kukabidhi meza 120 pamoja na mabenchi 240 ambazo watakalia wanafunzi 1200 kwaajili ya bwala la chakula Mkurugenzi mtendaji mkuu wa Air Tanzania Eng.Ladislaus Matindi amewataka watoto wakike kuchangamkia masomo ya sayansi ili kuweza kupata fursa mbalimbali zilizopo kwenye shirika hilo.
“niwaambie watoto wa kike fursa zipo Air Tanzani na ushahidi upo wakati tunaanza tulikuwa na rubani mmoja wa kike lakini kwa sasa tuna marubani kumi niwaambie tu fursa ipo na urubani nikazi ya wote na kazi ya urubani ni kazi ya umakini mkubwa sana na sayansi inaonesha wanawake ni watu wenye umakini mkubwa sana”Alisema Matindi.
Aidha Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ndege Tanzania amesema kuwa kampuni hiyo inatarajia kuongeza safari za ndege kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini ukiwemo mkoa wa Tanga.
kwaupande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ambaye ali mwakilisha Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe.jakaya Mrisho kikwete ameshukuru kwa msaada huo na kusema kuwa mkakati wa mkoa ni kuifanya shule hiyo kuwa moja ya shule bora hapa nchini kwani ni shule ya kwanza ya sekondari hapa nchini.
“jambo kubwa ambalo airTanzania inaweza kuendelea kusaidia shule hii kwa ali ni utayari wao wa kuanza kwa safari zao ndege katika kiwanja cha Tanga kama alivyo tangaza waziri wa uchukuzi kwani mkoa wa Tanga mambo mengi yanafunguka katika ujio wa bomba la mafuta”
“kwasasa kuna ongezeko kubwa la wageni wengi kuja hapa Tanga kutoka mataifa mbalimbali hivyo kuchagiza kukua kwa uchumi wetu hivyo kuna umuhimu mkubwa wa wezetu hawa wa AirTanzania kuanza safari zao hapa ili kuchangamkia fursa hiyo na kupata wateja wengi zaidia”.